Skip to main content

iKnowledge kijenzi ujuzi kwa Walimu(TAN)

Kuhusu kozi hii

iKnowledge ni mradi uliojikita katika kuleta TEHAMA na kuwezesha upatikanaji wa mtandao wa Satelaiti kwa shule zote kwa Tanzania bara na Zanzibar. Mradi unakusudia Kuunganisha, Kufikisha, na kutoa Mafunzo endelevu kwa shule za Tanzania kwa msaada wa washirika wa nje na ndani ya nchi.

Shule 100 za Msingi na shule 150 za Sekondari huwezeshwa kuwa na mtandao wa satelaiti na hupewa vifaa ili kuwawezesha walimu kutumia zana za kisasa zaidi za kufundishia madarasani. Kwa kuwepo miundombinu y a TEHAMA na muunganiko kupitia satelaiti, iKnowledge hutoa mafunzo ya kidijitali kwa walimu na maudhui ya kielimu kwa madhumuni ya kufundishia, ambayo hupimwa kwa kuangalia matokeo ya kujifunza.

Walimu hufikia mtandao wa intaneti kupitia satelaiti ya HYLAS 2 ya Avanti, amabyo imeenea kwa 100% Tanzania. Mtandao wa intaneti huwekwa na kuwezeshwa kupitia watoa huduma wa Raha waliopo nchini, wakati vifaa vya TEHAMA, mafunzo ya kidijitali na programu za kielimu hutolewa kwa ushirikiano wa Avanti Communications na Camara Education Tanzania. Programu hudhaminiwa na Shirika la Kimataifa la Anga la Uingereza (UK Space Agency's International Partnership Space Programme (IPSP)..

iKnowledge hukuza ufahamu na uelewa wa kidijitali wa walimu kupitia muundo endelevu wa ufudishaji wa "Mafunzo kwa Wakufunzi'. Hutoa maudhui ya kielimu kwa walimu kuweza kutumia moja kwa moja katika madarasa yao, kuboresha vizuri ushiriki wa elimu kwa wanafunzi.

Mahitaji

Wanakaribishwa katika kozi hii ya kujenga ujuzi:

-Walimu Tarajali, na

-Walimu, na

-Wakuu wa Shule, na

-Maafisa Elimu Wilaya.

  1. Course Number

    TE015-2-SW
  2. Classes Start

    Feb 02, 2017
  3. Classes End

    Mar 02, 2018
Enroll